
Chini ya laana ya dhambi asili yote ilipaswa kushuhudia kwa mwanadamu; tabia na matokeo ya uasi dhidi ya Mungu. Mungu alipomuumba mwanadamu alimfanya atawale dunia na viumbe vyote vilivyo hai. Muda wote Adamu alipoendelea kuwa mwaminifu kwa Mbingu, asili yote ilikuwa chini yake. Lakini alipoasi sheria ya kimungu, viumbe wa hali ya chini walikuwa katika uasi dhidi ya utawala wake. Hivyo Bwana, katika rehema yake kuu, angewaonyesha wanadamu utakatifu wa sheria yake, na kuwaongoza, kwa uzoefu wao wenyewe, kuona hatari ya kuiweka kando, hata kwa kiwango kidogo. PP 59, 60